| Kifo kifo kifo |
| Kifo kifo kifo |
|
| Nuru imepotea mbele hatuoni kiza |
| Kila kona machozi masikitiko |
| Mmh nafsi zanyongo'onyea |
| Huzuni moyoni unaumiza |
| Kitabu kizuri ndo kurasa ya mwisho |
| Vizuri havidumu |
| Nenda Magufuli umetimiza majukumu baba |
| Vizuri havidumu |
| Nenda jembe letu |
| Kuwacha mabarabara mahospitali |
| Wananchi ulivyowajali |
| Masikini kila hali Magufuli wetu |
| Upendo kwa wasanii kila mahali |
| Ulifurahi nasi ukatujali |
| Zile kofia kumbukumbu |
| Umefunga safari Magufuli wetu |
| Kina mama watafutwa na nani machozi |
| Wafungwa ulowasameheatawafuta nani machozi |
| Na vijana watatufuta nani machozi |
| Wazee wazee watawafuta nani machozi |
| Umeacha alama kumbukumbu isofutika |
| Pengo lako Magufuli sidhani kama litazibika |
| Moyo unalalama sisi bado twahuzunika |
| Umefanya kazi ngumu juu jaa |
| Basi nenda kupumzika jembe letu |
|
| Kifo kifo kifo |
| Kifo kifo kifo |
| Kifo kifo kifo |
| Kifo kifo kifo (Hauna huruma) |
| (Kwa nini kifo) |
|
| Machozi ya mama Samia yatafutwa na nani? |
| Machozi ya Kassim Majaliwa atayafuta na nani? |
| Machozi ya Bashiru atayafuta na nani? |
| Machozi ya Polepole atayafuta na nani |
| Machozi ya Kassim Majaliwa atayafuta na nani? |
| Machozi ya Watanzania atayafuta na nani? |
|